FT : Yanga 2-0 Mbao FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2018
FT : Yanga 2-0 Mbao FC
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga wameendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo msimu huu baada ya kuilaza Mbao FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Yanga iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na nia ya kuibuka na ushindi na hilo wamelifanikisha kwa asilimia 100.

Mabao ya Yanga yalipatikana kwenye kila kipindi ambapo bao la kwanza liliwekwa kambani na Raphael Daudi Lothi kwenye dakika ya 16 akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib Migomba.



Bao la pili la Yanga lilifungwa kwenye dakika za lala salama kipindi cha pili na Ajib akifunga bao zuri la 'kideoni'.



Ilikuwa ni krosi iliyomiminwa na Gadiel Michael kutoka upande wa kushoto ambayo iliwababatiza walinzi wa Mbao FC na kumkuta Ajib aliyefunga bao kwa staili ya 'pigo la ki-baiskeli'

Ajib ameendelea kudhihirisha ubora wake katika kikosi cha Yanga sasa akiwa amehusika kwenye mabao nane, sita ametengeneza na mawili amefunga.



Ushindi huo umeirudisha Yanga kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 16 ikiwa imeshuka dimbani mara sita tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’