Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imewasili visiwa vya Cape Verde tayari kwa mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019 dhidi ya wenyeji wao, Cape Verde.
Stars itachuana na Cape Verde keshokutwa Ijumaa nchini humo kabla ya timu hizo kurudiana kwenye mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumanne ijayo, Oktoba 16, 2018.
Stars iliondoka jijini Dar es salaam Alfajiri ya leo ikiwa na wachezaji 22 kwa usafiri wa ndege ya kukodi.
Wachezaji wanne wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta, Saimon Msuva, Farid Mussa na Shabaan Idd Chilunda wao walitangulia kuwasili mapema leo nchini humo.
Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amesema wamekwenda Cape Verde kuchukua alama zote tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za michuano hiyo zitakazofanyika nchini Cameroon mwezi Juni 2019.

ADVERTISE HERE