Timu ya Taifa ya Cape Verde imewasili Jumapili usiku tayari kwa mchezo dhidi ya Taifa Stars utakaopigwa Jumanne, Oktoba 16 kwenye uwanja wa Taifa.
Cape Verde inashika nafasi ya pili kundi L ikiwa imejikusanyia alama nne baada ya kuifunga Stars mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini mwao.
Mchezo huo wa Jumanne wa kusaka tiketi ya kutinga fainali ya michuano ya AFCON 2019 una umuhimu wa kipekee kwa kila timu.
Stars inahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kufuzu wakati ushindi utaisogeza Cape Verde karibu zaidi ya kukata tiketi.
Katika miaka ya hivi karibuni, Cape Verde imekuwa ikifuzu michuano hiyo ambapo ilifanya hivyo mwaka 2013 na 2015 na ikashindwa kufuzu mwaka 2017.
Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu kwa fainali za AFCON ni miaka 38 iliyopita.

ADVERTISE HERE