Claudio Deaguiar ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Cape Verde ambaye mwaka 2008 alifika nchini na kikosi cha timu hiyo kilichobugizwa mabao 3-1 na Tanzania.
Tukio kubwa ambalo mchezaji huyu analikumbuka mpaka leo ni kuwa baada ya mchezo huo mwaka 2008, alibadilishana jezi na winga wa Yanga Mrisho Ngasa ambaye mwenyewe amekiri 'aliwakimbiza' hasa.
Ngasa wakati huo yuko 'on fire' alifunga moja ya mabao ya Stars kwenye mchezo huo.
Claudio ambaye kwa sasa ni miongoni mwa makocha wa benchi la ufundi la Cape Verde, amekuja nchini na kikosi cha timu hiyo kitakachochuana na Stars kesho na ametamani kuonana na Ngasa uwanja wa Taifa.
Kituo cha runinga cha Azam ambacho kilifanya nae mahojiano Cape Verde kimeahidi kuwakutanisha wawili hao uwanja wa Taifa hapo kesho.
Ngasa ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Kitanzania ambao kutokana na uwezo wao, wamejijengea sifa na heshima nje ya Tanzania.
Sio jambo dogo kwa mchezaji kutoka Cape Verde kumkumbuka Ngasa aliyecheza nae miaka 10 iliyopita. Claudio amesema ameihifadhi jezi ya Ngasa mpaka leo.

ADVERTISE HERE