Zahera ahofia kurejea kwa Chirwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
22 Oct 2018
Zahera ahofia kurejea kwa Chirwa Yanga
Siku moja baada ya uongozi wa Yanga kumleta straika wake wa zamani Obrey Chirwa, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera ameonyesha hofu juu ya kusajiliwa kwa mchezaji huyo.

Zahera ambaye alifanya kazi na Chirwa siku za mwanzo za maisha yake Jangwani amesema anatambua uwezo wa mshambuliaji huyo lakini nidhamu yake inamtia shaka.

Zahera amesema tabia aliyoonyesha Chirwa kabla ya kutimka kwa kuigomea Yanga kucheza mechi nne kufuatia kuidai klabu hiyo ni kitu ambacho kilimkasirisha sana.

“Chirwa sio mchezaji mbaya, lakini sidhani kama anahitajika hapa alitugomea wakati nafika hapa alikataa kucheza mechi nne akisema anataka alipwe,” Zahera amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

“Tulimuhitaji wakati tunakwenda Algeria akagoma, lakini pia aligoma kwenda Shinyanga na Mbeya tukafungwa sidhani kama anatufaa kwa sasa.”

Inaelezwa kuwa bado kuna mvutano mkubwa baina ya kocha Zahera na viongozi wa Yanga iwapo mchezaji huyo arejeshwe kikosini au la.

Lakini wakati huo huo klabu ya Azam Fc imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Yanga inadaiwa kuwahi mchakato huo kwani tayari Azam Fc ilishafanya mazungumzo ya awali na Chirwa aliyetakiwa na Pluijm akaungane na Donald Ngoma.

Yanga ndio iliyomsafirisha mshambuliaji huyo kutoka nchini Misri kwa kumtumia tiketi ya ndege baada ya kuuelezea uongozi wa klabu hiyo juu ya nia yake ya kutaka kurejea Jangwani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →