Waziri Dk Mwakyembe akutanisha makundi yanayovutana kuhusu Uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2018
Waziri Dk Mwakyembe akutanisha makundi yanayovutana kuhusu Uchaguzi Yanga
Kikao cha wanachama wa Yanga kutoka makundi yanayovutana juu ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, mwafaka utajulikana baada ya siku mbili.

Kikao hicho ambacho kiliitishwa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kimemalizika na baadhi ya wanachama wakiridhishwa na kilivyoendeshwa.

Dk Mwakyembe amesema licha ya mvutano wa wanachama hao lakini kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa.

Mwakyembe amesema baaada ya kuzisikila pande zote amewaambia kwamba msimamo juu ya uchaguzi huo utatolewa baada ya siku mbili.

Amesema ameomba muda huo ili aweze kukutana na baadhi ya watendaji wa TFF na serikali kuweza kutoa muongozo wa serikali.

Aidha Dk Mwakyembe amewaambia wanachama hao pamoja na viongozi wao kwamba serikali haitaki kuona Yanga inatetereka hasa wakati huu ambao wanafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara

Nae Mzee Ibrahim Akilimali ambaye alishiriki kikao hicho amesema wameridhika na kikao hicho wanasubiri maamuzi wa Waziri Mwakyembe.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omari Kaya amesema wameridhika na uendeshwaji wa kikao hicho na sasa wanasubiri muongozo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’