Jana baada ya kutolewa kwa taarifa ya kuumia kwa 'mpishi' wa mabao ya Yanga Ibrahim Ajib, wengi waliamini timu hiyo isingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC.
Hata hivyo bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' kupitia mpira wa adhabu liliihakikishia Yanga ushindi muhimu.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema timu yake ilicheza vizuri na ilistahili kupata ushindi huo.
Zahera amesema anatambua Ajib ni mchezaji wao wanaemtegemea zaidi katika kutengeneza mabao lakini kukosekana kwake halikuwa tatizo kwao
"Tumecheza vizuri. Tumeweza kufanya majaribio mengi langoni kwa KMC. Mipira minne imegonga mwamba, tulikosa bahati tu lakini tungeweza kushinda kwa mabao mengi zaidi," amesema Zahera
"Nawapongeza KMC ni timu nzuri. Walikosa umakini tu walipofika langoni. Lakini ni timu ambayo ingefaa iwe katika nafasi za juu sana kwenye msimamo wa ligi"
Ajib aliondolewa kikosini baada ya kupata maumivu ya mgongo wakati Yanga ikijiandaa na mchezo huo

ADVERTISE HERE