Tambwe 'amemiss' kuifunga Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2017
Tambwe 'amemiss' kuifunga Simba
Mshambuliaji hatari wa Yanga Amissi Tambwe amesema ana hamu kubwa na siku ya August 23, keshokutwa Jumatano ambapo kutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya mabingwa wa VPL Yanga na mabingwa wa ASFC, Simba.

Tambwe amenukuliwa na moja ya magazeti ya burudani leo akisema anataka kuweka rekodi nyingine kwa kuifunga Simba, timu yake ya zamani kwa mara ya nne.

Mpaka sasa Tambwe amecheza michezo mitano dhidi ya Simba na amefunga katika michezo mitatu.

"Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni", amesema.

"Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati".

"Endapo nitapata nafasi ya kuanza hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya kuifunga mara nyingi," alisema Tambwe.

Jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri Tambwe alicheza kwa dakika 35 na kocha George Lwandamina akamtoa ikiaminika alifanya hivyo ili kumuepusha asije akaumia kuelekea mpambano huo.

Tangu atue Yanga misimu mitatu iliyopita, Tambwe amekuwa na rekodi nzuri ya kuzifumania nyavu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’