Viongozi wa Matawi Yanga wapinga maamuzi ya BMT

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2018
Viongozi wa Matawi Yanga wapinga maamuzi ya BMT
Viongozi wa matawi wa klabu ya Yanga kwa pamoja wamepinga maamuzi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya kuitaka klabu hiyo ifanye uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo ziko wazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa matawi wa klabu hiyo Boaz Ikupilika amesema kwamba viongozi wa matawi katika kikao chao kilichofanyika jana kimeliagiza Baraza la wadhamini kuitisha mkutano mkuu wa dharula ili kupata ukweli wa Mwenyekiti wao Yusuph Manji.

Ikupilika amesema kwamba mbali na hilo pia viongozi hao wamekataa uchaguzi kusimamiwa na TFF kwa sababu kamati yao ya uchaguzi iko hai.

Juzi BMT iliiagiza Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi na uchaguzi huo usimamiwe na TFF ikieleza kamati ya uchaguzi ya yanga haijitoshelezi.

Baraza hilo pia liliagiza wanachama wote wenye kadi tofauti kwenda kwenye matawi yao kujisajili ndani ya wiki tatu kuanzia juzi.

BMT ikaiagiza TFF kuchagua tarehe ya uchaguzi na tarehe yenyewe itangazwe mwezi huu

BMT iliagiza pia kuwa uchaguzi huo uhusishe nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga baada ya kujiridhisha kuwa Yusufu Manji anayetambuliwa na wanachama kama Mwenyekiti, hajarejea klabuni hapo
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’