Hili la Chirwa Zahera hapaswi kulaumiwa

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
8 Nov 2018
Hili la Chirwa Zahera hapaswi kulaumiwa
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa ametambulishwa rasmi katika klabu ya Azam Fc na ataanza kuitumikia timu hiyo wiki ijayo dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Chirwa alitumiwa tiketi ya ndege na viongozi wa Yanga kuja nchini asajiliwe na mabingwa hao wa kihistoria baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri.

Hata hivyo kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alipinga bila kificho usajili wa mshambuliaji huyo akieleza kutofurahishwa na matukio yake ya utovu wa nidhamu.

Zahera alipata nafasi ya kufanya kazi na Chirwa mwishoni mwa msimu uliopita na alikerwa na tabia ya migomo aliyokuwa akifanya.

Zahera alisema Chirwa aligoma kuichezea Yanga katika michezo mitano ya mwishoni mwa msimu akishinikiza alipwe stahiki zake.

Chirwa aligoma kusafiri na kikosi cha Yanga kilipokwenda kuivaa USM Alger katika mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho hatua ya makundi na Yanga kufumuliwa mabao 4-0

Hayo ni matukio ambao Zahera aliyashuhudia, lakini mashabiki wa Yanga nadhani wanamfahamu zaidi Chirwa na vituko vyake.

Kuna wakati msimu uliopita alirejea kwao Zambia kuendelea na shughuli za kilimo wakati huku ligi inaendelea!

Ukweli ni kwamba Zahera aliona mbali kumkataa Chirwa kurejea Yanga kwa kuwa ni mchezaji ambaye sio mvumilivu.

Chirwa sio mchezaji ambaye anaweza kuvumilia mshahara au madai yake yoyote yanapocheleweshwa. Kimsingi hawezi kulaumiwa kwa kuwa ni haki yake.

Lakini inapotokea timu inakabiliwa na 'ukata' yapaswa wachezaji kuifahamu hali hiyo na kujitolea kufanya kazi kwani siku zote madai huwa yanalipwa japo yanaweza kuchelewa.

Yanga bado haina hali nzuri ya kiuchumi. Bado mishahara ya wachezaji hailipwi kwa wakati.

Juzi zimeripotiwa habari kwenye magazeti kuwa kuna wachezaji walikacha mazoezi ikielezwa wanashinikiza walipwe madai yao ya mishahara na marupurupu mengine.

Chirwa asingeweza kuvumilia hali hiyo. Lazima angegoma, tena wakati ambao anahitajika sana.

Kwa hali ya kiuchumi ilivyo Yanga inahitaji wachezaji wa aina tofauti kabisa.

Wachezaji ambao wanaweza kuvumilia mishahara yao inapochelewa. Wachezaji ambao wanaweza kuwaelewa viongozi hasa timu inapokumbwa na wakati mgumu.

Mashabiki wa Yanga kuendelea kumlaumu Zahera baada ya Chirwa kutua Azam Fc ni kumuonea tu.

Yeye alisoma alama za nyakati na akajua kwa hali ilivyo Yanga Chirwa lazima angeleta usumbufu kama kawaida na kumuharibia mipango yake.

Wanachama na Mashabiki wa Yanga wanapaswa kuusumbua uongozi wa timu yao ukubali kufanya mabadiliko ili timu iondokane na hali iliyonayo sasa.

Mchawi wa Yanga sio Zahera, wachawi ni wale ambao wamekuwa wakichelewesha maendeleo ya timu na kuifanya kuwa maskini ikitegemea kuchangiwa na wanachama na mashabiki
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’