Kuuli aiponda TFF ya Karia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2018
Kuuli aiponda TFF ya Karia
Siku chache baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumfungia maisha kutojihusisha na masuala ya soka, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Revocatus Kuuli, ameibuka na kulichambua shirikisho hilo, huku akidai kuwa uongozi huo wa sasa umeanguka mapema.

Kuuli, alisema mambo yanayoendelea sasa ndani ya TFF yanaonyesha namna ambavyo uongozi wa Rais Wallance Karia ulivyokosa njia mpaka kufikia hatua Ligi Kuu imekosa mdhamini.

Kuuli aliyasema hayo wakati alipoulizwa mtazamo wake baada ya kufungiwa na TFF wakati tayari alikuwa ameandika na kuwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi yake.

"Ni mambo ya kushangaza na ndio maana sikwenda kwenye kikao cha Kamati ya Maadili, nilishajiuzulu nafasi yangu muda mrefu sasa naitwaje kwenye kamati hiyo?" Alihoji Kuuli.

Aidha, alisema kilichotokea kwake alishakiona na kuamua kujiondoa mapema.

"Haya mashtaka niliyopewa yalipangwa muda mrefu na ndio maana niliamua kujiuzulu mapema, nisingeweza kufanya kazi na watu wa aina hii," aliongeza kusema Kuuli.

Kuuli alijiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kile alichokidai kuingiliwa kazi yake na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau.

Tofauti ya viongozi hao iliibuka wakati wa mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba ambapo Kuuli alitaka uchaguzi huo usimame kupisha mabadiliko ya katiba yao, huku Kidau akiagiza taratibu ziendelee.

Hata hivyo, Rais wa TFF, Karia akizungumza juzi, alisema kimsingi adhabu aliyopewa Kuuli imetolewa na chombo halali kulingana na makosa aliyoyafanya.

Alisema hataki kulizungumzia suala hilo kwa kuwa wamejielekeza kwenye kuendeleza soka na si malumbano yasiyokuwa na tija.

"Adhabu imeshatoka, niacheni nifanye kazi ya kuendeleza soka letu, suala hili limeshapita, kama alifanya vizuri wakati wa uchaguzi ulioniweka madarakani hiyo haimaanishi siwezi kumchukulia hatua pindi anapokosea, Kuuli amechukuliwa hatua kulingana na makosa yake", alisema Karia.<

Kuuli, anakumbukwa kusimamia na kuratibu mchakato wa uchaguzi uliomuingiza madarakani Rais Karia, huku akisimamia kanuni ya ulazima wa kufanyiwa usahili wagombea wote kabla ya uchaguzi huo.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’