Yanga, TFF zakubaliana uchaguzi utafanyika January 13 2019

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2018
Yanga, TFF zakubaliana uchaguzi utafanyika January 13 2019
Uongozi wa klabu ya Yanga umefikia makubaliano na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) juu ya uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika January 13, 2019.

Uchaguzi huo wa kujaza nafasi zilizowazi utafanyika kama ulivyopangwa ambapo Yanga na TFF zimekubaliana kuwa Kamati zote mbili za uchaguzi(ya TFF na Yanga) zitashirikiana kuusimamia uchaguzi huo

Katika tamko lililotolewa na TFF mbele ya waandishi wa habari mapema leo, uchaguzi huo utafanyika bila ya kujali kupingwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga

Aidha, kwa wale ambao wamekuwa wakisisitiza kumtambua Yusufu Manji kama Mwenyekiti wa Yanga, wameshauriwa wamshawishi na hata kwenda kumchukulia fomu ili aweze kugombea tena nafasi hiyo

Uchaguzi huo utahusisha nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi nne za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji

Katika hatua nyingine, Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga imemteua Thobias Lingalangala kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo hadi uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo utakapofanyika Januari 13.

Lingalangala amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyotangazwa na Kamati ya uchaguzi ya TFF na fomu zimeanza kutolewa rasmi leo ofisi za TFF na Klabuni Yanga.

Gharama za fomu nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni laki mbili na Wajumbe ni laki moja
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’