Zoezi la utolewaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Yanga linatarajiwa kufungwa leo Jumatatu, Novemba 19 2018 ambapo mpaka juzi wagombea 22 walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu.
Zoezi hilo ambalo awali lilikuwa lifungwe Novemba 14, liliongezwa kwa siku tano ili kutoa nafasi kwa wagombea wengi kujitokeza.
Hadi juzi jioni, wagombea wanne walikuwa wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti ambao ni Dr Jonas Tibaroha, Mbaraka Igangula, Yono Kevele na Titus Osoro.
Kevele na Osoro walichukua fomu mbili, ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kila mmoja ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesema watatambua fomu moja pekee itakayojazwa na wagombea hao mara watakaporudisha.
Wajumbe waliojitokeza ni Mussa Katabalo, Salim Seif, Benjamini Jackson, Pindu Luloya, Silvester Haule, Hamad Islam, Shaffii Amri, Said Baraka, Dominic Francis, Ally Msigwa, Leonard Malongo, Salum Chota, Ramadhan Said, Geofrey Mwita, Faustine Mabula, Frank Kalokola na Arafati Haji

ADVERTISE HERE