Kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima amekanusha taarifa zilizochapishwa katika magazeti mengi ya burudani siku chache zilizopita kuwa amesajiliwa na klabu ya Simba, mahasimu wa Yanga.
Niyonzima ambaye yuko mapumziko nchini kwao Rwanda baada ya kuitumikia timu yake ya Taifa amekiri kupokea ofa kutoka kwa Simba sambamba na timu yake ya sasa Yanga.
Hata hivyo amesema hatakurupuka kufanya maamuzi kwa kuwa bado ana mkataba na klabu ya Yanga unaomalizika mwishoni mwa mwezi huu.
"Mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga kwa kuwa mkataba wangu bado haujamalizika," amesema Niyonzima.
Γ’β¬ΕHivi karibuni watu watajua ni timu gani nitacheza msimu ujao lakini kwasasa, sijasaini timu yoyote," amesema.
Karibuni vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti ya burudani yameripoti kuwa kiungo huyo amesajiliwa Simba kwa dau la Milioni 100

ADVERTISE HERE