Kabwili, Ninja na Boxer waongeza nguvu Shinyanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2018
Kabwili, Ninja na Boxer waongeza nguvu Shinyanga
Mlinda lango Ramadhani Kabwili, walinzi Abdallah Shaibu 'Ninja' na Godfrey Paulo 'Boxer' wametua mkoani Shinyanga kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kinachoshuka uwanja wa CCM Kambarage leo kuumana na Mwadui FC.

Wachezaji hao walikuwa kwenye timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 ambayo juzi iliondoshwa kwenye michuano ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 kwa ngazi ya vijana licha ya kushinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Burundi baada ya kufungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza.

Kuwasili kwa wachezaji hao, kumeongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga ambacho kitawakosa nahodha Kelvin Yondani na mlinda lango Beno Kakolanya ambao hawakusafiri kwa sababu binafsi.

Yanga imedhamiria kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo ili kuendeza rekodi ya kutofungwa msimu huu pia kuendeleza presha kwa wapinzani wake katika mbio za ubingwa, Azam fc na Simba
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’