FT : Kagera Sugar 1-2 Yanga, ushindi wa pili ugenini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2018
FT : Kagera Sugar 1-2 Yanga, ushindi wa pili ugenini
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga leo wameendeleza rekodi ya ushindi ugenini kwa asilimia 100 baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa dimba la Kaitaba.

Haritier Makambo ambaye amerejesha makali yake ya kupachika mabao, aliitanguliza Yanga kwenye dakika ya 21 kwa bao safi la kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Haji Mwinyi.





Kagera Sugar walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 32 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ramadhani Kapera baada ya mshambuliaji huyo kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari

Katika kipindi cha pili ni Yanga iliyorejea ikiwa na kasi ya kusaka bao la ushindi.

Yanga iliongeza kasi zaidi baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mwinyi Zahera aliyewatoa Makamnbo aliyepata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajib, Maka aliyetoka kumpisha Raphael Daudi na Haji Mwinyi aliyempisha Deus Kaseke.

Alikuwa ni Lothi aliyeihakikishia Yanga alama tatu muhimu kwenye dakika ya 74 alipounganisha kwa kichwa mpira aliotengenezewa na Deus Kaseke kutoka krosi ya Paulo Godfrey 'Boxer' aliyekuwa na mchezo mzuri sana.

Mlinda lango Ramadhani Kabwili leo ameonyesha ukomavu na kudhihirisha kuwa yeye ni chaguo sahihi la kulinda lango mbele na Klaus Kindoki baada ya kuokoa mashambuliz ya hatari wakati mchezo huo ukielekea ukingoni

Matokeo hayo yameikita Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imefikisha alama 32, alama tano mbele ya Simba mabayo iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 12.

Yanga pia iko nyuma ya Azam Fc kwa alama moja tu huku pia ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa utaipeleka Yanga kileleni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’