Mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mwadui Fc akishindwa kuendelea na mchezo huo katika kipindi cha pili baada ya kuumia kwenye kipindi cha kwanza.
Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amesema hali ya beki huyo inaendelea vizuri ambapo anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi baada ya timu kurejea jijini Dar es salaam.
βAnaendelea Vizuri, baada ya kufika Dar es Salaam, kesho tutafanya vipimo vya mwisho lakini Hakuna shaka kuwa wakati wowote anaweza kurejea uwanjani," amesema Dk Bavu
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Mwanza usiku huu wa Jumatatu Nov 25 kwa usafiri wa ndege kurejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Alhamisi ijayo katika uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE