Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumlivu pale baadhi ya wachezaji wanapocheza chini ya viwango vyao kwa kuwa ni jambo la kawaida.
Zahera amedai kushangazwa na mashabiki hao kumshushia lawama Heritier Makambo mshambuliaji wa timu hiyo kinara wa mabao alipocheza chini ya kiwango michezo michache iliyopita.
Lakini sasa imekuwa tofauti ambapo mshambuliaji huyo amekuwa akipongezwa na kushangiliwa kila anapopita baada ya kurejea katika ubora wake wa kupachika mabao.
"Mashabiki wamekosa uvumilivu kwa kushindwa kuwapa muda wachezaji waweze kuonyesha ubora wao," amesema Zahera.
"Kama ilivyo kwa Kindoki sasa, kuna wakati Makambo alicheza chini ya kiwango na wengi walimshambulia na kusema sio mchezaji mzuri na hana sifa ya kucheza Yanga
"Lakini sasa baada ya kuanza kufunga kila mmoja anamshangilia na kumpongeza kila anapopita"
"Mashabiki hawafahamu kuwa hata kwa wachezaji siku hazifanani. Kuna wakati wanaweza kucheza chini ya kiwango."
"Hata Lionel Messi kuna wakati hafungi. Cristiano Ronaldo alipohamia Italia alicheza michezo mitano bila ya kufunga
"Ninawafahamu vizuri Kindoki na Makambo na sina shaka na uwezo wao. Katika ligi kuu ya Congo inayozihusisha timu kama TP Mazembe Makambo alifunga mabao 16 kwenye michezo nane"
"Sasa mchezaji huyo ndio aje ashindwe kufanya vizuri kwenye ligi ya hapa Tanzania?," alihoji Zahera

ADVERTISE HERE