Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Clifford Mario Ndimbo amesema mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga utapigwa kesho Alhamisi Novemba 29 uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kama ulivyopangwa.

Awali ilitolewa taarifa kuwa mchezo huo ungechezwa jijini Dar es salaam na ule wa marudiano ndio ungepigwa jijini Tanga mwezi wa pili mwakani.
JKT Tanzania ilipinga mabadiliko hayo ya ratiba ikitaja sababu kuwa ilikuwa imefanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo kufanyika mkoani Tanga.
Yanga sasa inalazimika kusafiri kwenda mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo huo kisha kuunganisha mkoani Mbeya kuikabili Tanzania Prisons Disemba 03.
TAARIFA MPYA
Mchezo wa kesho utapigwa uwanja wa taifa, mchezo wa marudiano ndio utapigwa jijini Tanga, Februari 09

ADVERTISE HERE