Waziri Dk Mwakyembe kupewa taarifa ya uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2018
Waziri Dk Mwakyembe kupewa taarifa ya uchaguzi Yanga
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe leo atakutana na Kamati ya Shirikisho la soka nchini inayohusika na maandalizi ya mashindano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17, yatakayofanyika mwakani.

Katika kikao hicho pia Dk Mwakyembe atapokea taarifa kuhusu maendeleo ya mchakato wa uchaguzi wa Yanga wa kujaza nafasi zilizowazi unaotarajiwa kufanyika January 13 2019.

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi huo ambao mpaka sasa umesimamiwa na Kamati ya uchaguzi ya TFF pekee bila ya klabu ya Yanga ambao ndio wahusika wakuu kushiriki.

Yanga imeshikilia msimamo wa kutaka uchaguzi huo usimamiwe na Kamati yake ya uchaguzi lakini pia ikipinga uchaguzi kwa nafasi ya Mwenyekiti baada ya Mwenyekiti wake Yusufu Manji kurejea.

Jana Dk Mwakyembe alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akisema leo Jumatano wakati akikutana na Kamati ya maandalizi ya mashindano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17, yatakayofanyika mwakani hapa nchini pia atapokea taarifa kuhusu maendeleo ya mchakato wa uchaguzi wa Yanga.

"Mimi huwa sitaki kusikia mambo ya barabarani nataka vitu viwekwe mezani ili kama kuna changamoto tuitatue.

"Mpaka sasa bado hawajaniletea taarifa na kesho (leo) kabla ya kikao cha Afcon nina uhakika watanipa taarifa kuhusu mchakato wa uchaguzi ili kama kuna changamoto ziweze kutatuliwa."

"Sidhani kama suala la Yanga ni gumu ni jambo la kutumia hekima na busara ili tuweze kusonga mbele," alisema Mwakyembe
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
22m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’