Yanga yapania kuiondoa kileleni Azam Fc kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2018
Yanga yapania kuiondoa kileleni Azam Fc kesho
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga kesho wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara ukiwa ni mchezo wa kiporo.

Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa imeshuka dimbani mara 12 na kujikusanyia alama 32, itaweza kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kama itaibuka na ushindi au hata kutoka sare kesho.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mcongomani Mwinyi Zahera amesema timu yake imejiandaa kikamilifu na imejiwekea malengo ya kuondoka na alama zote tatu.

Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeruhi na sababu nyinginezo, Zahera amesema hana wasiwasi na kikosi chake kwani kimesheheni wachezaji wenye uwezo.

"Tumejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo wa kesho. Kama ilivyo kawaida, tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa na malengo ya kuondoka na alama zote tatu," amesema Zahera.

"Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, tumeweza kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo huo. Tutaingia na lengo letu kuu la ushindi kama tulivyofanya katika michezo mingine"

Ushindi kesho utaipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi lakini pia utaifanya timu hiyo izidi kuitimulia vumbi Simba iliyo nafasi ya tatu na alama 27

Kama Yanga itashinda kesho itaizidi Simba kwa alama nane.

Viingilio vya mchezo huo;

VIP A - 15,000/-
VIP B na C - 10,000/-
Mzunguuko - 5,000/-
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
36m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’