Kakolanya akizubaa tu, Kabwili anachukua namba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2018
Kakolanya akizubaa tu, Kabwili anachukua namba
Mlinda lango Beno Kakolanya hakusafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda mkoani Mbeya kuikabili Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa kesho Jumatatu dimba la Sokoine.

Kakolanya ameachwa jijini Dar es salaam ikielezwa ni majeruhi ingawa pia anahusishwa na tetesi za mgomo ambazo zimetawala kwenye mitandao ya kijamii.

Juzi ziliibuka taarifa kuwa mchezaji huyo ameomba kuvunja mkataba wake, klabu ya Simba ikihusishwa kuwa nyuma ya mpango huo ili iweze kumsajili.

Hata hivyo Kakolanya amekanusha tetesi hizo na kusisitiza mkataba wake na Yanga utamalizika mwaka 2020.

Kukosekana kwake katika kikosi cha Yanga wakati huu hakuonekani kama ni tatizo kwani kinda Ramadhani Kabwili anafanya vizuri sana.

Kabwili anatarajiwa kucheza mchezo wake wa nne kesho mbele ya Klaus Kindoki ambaye amekuwa mlinda lango namba tatu

Kama Kabwili ataendelea kufanya vizuri ataweza kumpa changamoto Kakolanya na akizubaa 'bwa mdogo' atamuweka benchi moja kwa moja
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’