Jana Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Michael Wambura alitinga Makao Makuu ya Shirikisho hilo kuwasilisha nyaraka ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyomrejesha kwenye nafasi yake.
Hata hivyo alishindwa kuonana na viongozi waandamizi wa Shirikisho hilo ambao hawakuwepo ofisini wakati alipowasili majira ya saa tano asubuhi
Wambura aliwasilisha nyaraka hizo ambazo zilipokewa na msimamizi wa ofisi aliyefahamika kwa jina la Ratifah baada ya viongozi wakuuu akiwamo Rais, Wallace Karia na Katibu Mkuu, Wilfred Kidao, kukosekana.
Baada ya kupokewa kwa nyaraka hizo, Wambura aliwaambia waandishi wa habari kuwa safari yake imefanikiwa licha ya kukosekana kwa viongozi wakuu.
“Sihitaji kuwaomba kurudi ofisini, mimi nilichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TFF, wao wakanifungia kujihusisha na soka. Nimekwenda mahakamani wametengua uamuzi wa mimi kufungiwa, hivyo nimerudi ofisini. Nimekuja hapa kuwafahamisha nimerudi na bado nipo, alisema Wambura
“Nimekabidhi na imepokelewa kwa kusainiwa, lakini sikukuta viongozi labda Mkurugenzi wa Fedha na wafanya kazi wengine wa chini hata hivyo lengo langu lilikuwa kuzileta hapa nyaraka hizi ili kukwepa visingizio vya kupewa nyaraka hizo.
“Hukumu ya Mahakama Kuu hakuna wa kuipinga kwa mujibu wa Katiba ya nchi, lakini hata hivyo lazima nikiri kwamba kuna tatizo ndani ya katiba ya TFF hivyo nitajitahidi kuonana na Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, kujadili kuhusu jambo hili.
“Tatizo hili ni la muda mrefu kwamba katiba yetu ya TFF inatakiwa kurekebishwa baadhi ya vifungu ambavyo vitafanya walalamikaji wasiende Mahakamani.
“Kulitakiwa kuwepo kamati ya usuluhishi kikatiba ambayo itakuwa ikisikiliza watakaohisi wameonewa katika hukumu kama iliyonikuta,” alisema Wambura.

ADVERTISE HERE