Mmiliki wa klabu ya African Lyon Rahim Kangezi Zamunda amesema kiungo Haruna Moshi 'Boban' aliyesajiliwa na Yanga alikuwa akiwaniwa na AFC Leopards ya Kenya.
Zamunda ambaye ndiye aliyemrudisha Boban nchini kutoka Ufaransa amesema Boban bado ana kiwango cha hali ya juu na anaamini ataitwa tena kuitumikia timu ya Taifa.
Akizungumzia kuhusu mchezaji huyo aliyekuwa tegemeo kwa klabu ya African Lyon kusajiliwa na Yanga, Zamunda amesema amefurahi kwa Boban kupata nafasi hiyo kwani kwa uwezo wake ni timu anayostahili kucheza.
Zamunda alisema alikuwa tayari kumruhusu Boban akajiunga na Yanga hata bure kwani anaamini kwa kufanya hivyo atakuwa amemsaidia mchezaji mwenyewe lakini pia akiwa katika klabu ya Yanga ataweza kupata nafasi nyingine ya kulitumikia Taifa.

ADVERTISE HERE