Yanga yaikaribisha Tukuyu Stars Dar kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2018
Yanga yaikaribisha Tukuyu Stars Dar kombe la FA
Tukuyu Stars ilifanikiwa kuiondosha Ihefu kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya kombe la FA (ASFC) na sasa itacheza na Yanga kwenye raundi ya tatu.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na TFF, michezo ya raundi ya tatu itapigwa kati ya Disemba 21-24 ambapo mchezo kati ya Yanga dhidi ya Tukuyu Stars unatarajiwa kupigwa Disemba 24 katika dimba la Taifa.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema mashindano hayo wanayachukulia uzito sawa na ligi kuu hivyo wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kusonga mbele hatua inayofuata.

Yanga iliyokuwa ya kwanza kutwaa taji la FA lilipoanzishwa msimu wa 2015-16, itatinga hatua ya 32 bora (raundi ya nne) kama itaifunga Tukuyu Stars.

Msimu uliopita Yanga iliondoshwa kwa matuta na Singida United kwenye hatua ya robo fainali baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1

Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’