Uchaguzi ulete mabadiliko ya kweli Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
24 Dec 2018
Uchaguzi ulete mabadiliko ya kweli Yanga

Ili kuwa na maendele endelevu, ni wazi Yanga inahitaji kwenda na wakati, kukubali kufanya uchaguzi ni moja ya hatua muhimu.

Ingawa Wana Yanga wanaona hawakutendewa haki na Serikali kwa kuwalazimisha uchaguzi wao usimamiwe na TFF, ikumbukwe Serikali ilitoa siku 60 kwa Yanga kufanya uchaguzi wao wenyewe ikashindikana, zikaongezwa nyingine 75 ikashindikana.

Jambo lililokuwa linakwamisha mchakato huo ni nafasi ya Mwenyekiti ambapo kila wakati ilipoelezwa kuwa Yusufu Manji angerejea klabuni hapo mambo mengine yote yalisimama.

Ni zaidi ya miezi sita imepita tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga na tangu wakati huo ni kama Yanga haijapiga hatua yoyote katika ngazi ya uongozi zaidi ya mvutano wa wale wanaomtaka Manji na wale wanaotaka uchaguzi.

Lakini sasa jambo hilo limemalizwa na Serikali na uchaguzi wa Yanga utafanyika Januari 13 2019. Ni vyema na viongozi wa Yanga nao wameridhia uchaguzi huo kufanyika na kuahidi kushirikiana na TFF kuusimamia.

Wengi wanataka kuiona Yanga ikiendeshwa kwa mfumo wa kisasa kama ilivyo kwa watani zao. Ili kulifanikisha hilo hatua ya kwanza ni kuwa na viongozi watakaoweza kusimamia mchakato huo.

Ni vyema wanachama wa Yanga wakajipa nafasi ya kuwasikiliza wagombea waliojitokeza hasa kuwania nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ili waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya uchaguzi Januari 13.

Wagombea watatu wanaowania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Jonas Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Mbaraka Igangula na Erick Ninga wakati wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Titus Osoro, Salim Chota, Yono Kevela na Pindu Luhoyo

Yanga sasa inafanya vizuri ni vyema mafanikio haya yakalindwa kuhakikisha timu inarejesha heshima yake. Migogoro inaweza kuharibu mara moja mafanikio haya yaliyopiganiwa kwa jasho na damu na wachezaji, benchi la ufundi na vongozi waliopo Yanga.

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’