Zahera kuiwahi Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2018
Zahera kuiwahi Mbeya City

Baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 kombe la FA dhidi ya Tukuyu Stars leo, mwishoni mwa wiki hii kikosi cha Yanga kinakabiliwa na mchezo wa kufunga mwaka 2018 dhidi ya Mbeya City utakaopigwa dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atauwahi mchezo huo wa ligi unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

Zahera anatarajiwa kutua nchini siku ya Jumatano Disemba 26 kutoka Ufaransa alikokwenda kushughulikia masuala yake binafsi ya kibiashara.

Kufuatana na ushauri wa kocha huyo kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka siku ya Alhamisi Disemba 27 kwa usafiri wa ndege.

Zahera amewataka mashabiki wa Yanga kuichangia timu hiyo ili kuhakikisha inakwenda mkoani Mbeya kwa ndege kama ilivyopanga

Kocha huyo aliyeonyesha mapenzi makubwa kwa Yanga amesema yeye pia atachangia kiasi cha pesa kitakachopungua ili kuhakikisha Yanga inakwenda Mbeya kwa Ndege

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’