Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara imeanza leo kwa michezo saba kupigwa kwenye viwanja mbalimbali.
Watani walikuwa kwenye dimba la Uhuru na wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting iliyowakosa wachezaji wake saba wa kikosi cha kwanza.
Ukiacha mchezo huo, michezo mingine iliyopigwa leo, Azam FC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC. Singida United imeanza kwa kuchapwa mabao 2-1 na Mwadui FC.
Mbao FC licha ya kupoteza wachezaji wake wote muhimu imefanikiwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0 mkoani Kagera.
Mtibwa Sugar imeilaza Stand United bao 1-0 wakati Njombe Mji imechapwa mabao 2-1 na Tanzania Prisons. Mbeya City imeilaza Majimaji bao 1-0.
Yanga itashuka dimbani kesho Jumapili kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Lipuli. Ushindi mnono ni muhimu katika mchezo huo ili kwenda sambamba na watani ambao wamepata mteremko leo.

ADVERTISE HERE