Zahera kuigharimu Simba kwa AS Vital Club

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2018
Zahera kuigharimu Simba kwa AS Vital Club

Florent Ibenge kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya DR Congo ndiye Mkufunzi wa timu ya AS Vital Club ambayo imepangwa na Simba kundi D kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi.

Mwinyi Zahera kocha wa Yanga anafanya kazi pamoja na Ibenge katika timu ya Taifa ya DR Congo yeye akiwa kocha msaidizi. Ibenge na Zahera wanafahamika kuwa marafiki wa muda mrefu

Uwepo wa Zahera hapa nchini huenda ukamnufaisha Ibenge na timu yake ya AS Vital hasa timu hiyo itakapokutana na Simba katika michezo ya hatua ya makundi inayoanza mwezi ujao.

Mbali na AS Vital Club katika kundi D pia zimo Al Ahly na Soura ya nchini Algeria ambayo anacheza mshambuliaji Thomas Ulimwengu.

Al Ahly ilicheza fainali ya ligi ya mabingwa michuano iliyomalizika mwaka huu wakati AS Vital wao walicheza fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho iliyomalizika mwezi uliopita.

Mafanikio anayopata Ibenge na kikosi chake cha AS Vital ndio yanayomhamasisha Zahera ambaye nae anataka kuhakikisha anaifikisha Yanga kwenye ngazi za juu katika michuano ya CAF.

Hakuna shaka Zahera ataifikisha Yanga mbali katika michuano hiyo msimu ujao kama itafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’