Kheri ya mwaka 2019 kwa Wana Jangwani wote

Admin By Admin
β€’
31 Dec 2018
Kheri ya mwaka 2019 kwa Wana Jangwani wote

Tunawatakia kheri ya mwaka 2019, wadau wa Mwana Jangwani, mashabiki na Wanachama wa klabu ya Yanga wakati tukiwa ukingoni wa mwaka 2018.

Wana Jangwani tunayo kila sababu ya kujivunia mafanikio iliyopata timu yetu kwa kufunga mwaka 2018 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Mwaka 2018 tumeumaliza kwa furaha licha ya kuwa sehemu kubwa ya mwaka huo ulijawa na machungu.

Mwaka 2018 tulipoteza ubingwa wa ligi kuu kwa wapinzani wetu Simba huku timu ikikumbwa na changamoto za kiuchumi.

Viongozi wengi wa Yanga wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti na wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji walijiuzulu nafasi zao kutokana na changamoto hizo.

Mwaka huo pia Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa aliiachia nafasi yake kutokana na matatizo ya kiafya yaliyomlazimu kwenda India kutibiwa.

Mwaka 2018 Yanga ilimpoteza aliyekuwa kocha wake George Lwandamina aliyerejea klabu ya ZESCO kutokana na hali ngumu lakini ikampata kocha Mwinyi Zahera ambaye kimsingi amehusika kwa kiasi kikubwa kuirejesha furaha ya Wana Jangwani.

Suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi nalo hivi karibuni nusura liharibu mustakabali wa timu lakini ni jambo jema kuona Wana Yanga wameridhia kufanyika kwa uchaguzi huo Januari 13 2019.

Kama tulivyomaliza mwaka 2018, Wana Jangwani tuendelee kushirikiana pamoja na viongozi wa Yanga ili kuhakikisha tunamaliza nusu iliyobaki kurudisha ubingwa Jangwani mwaka 2019.

HERI YA MWAKA MPYA...

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’