Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga leo usiku wanashuka katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kuikabli KVZ kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya kombe la Mapinduzi kundi B.
Katika kundi hilo, jana Azam Fc ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Jamhuri
Yanga iliwasili visiwani Zanzibar jana mchana tayari kushiriki michuano hiyo ambayo mwaka inashirikisha timu kutoka Tanzania pekee.
Mashabiki wa timu hiyo watakuwa na shauku ya kuona uwezo wa kikosi chao cha vijana ambacho kimepewa jukumu la kushiriki michuano hiyo kikiongezewa nguvu na wachezaji watano wa kikosi cha kwanza.
Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila ambaye ndiye bosi wa kikosi cha Yanga katika michuano hiyo, amesema wamekwenda Zanzibar kushindana.
ADVERTISE HERE