Baada ya hapo jana kulazwa mabao 3-0 na Azam Fc, kikosi cha Yanga kitakuwa na nafasi ya kuweka hai matumaini ya kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi kama kitaweza kupata ushindi dhidi ya Malindi Fc katika mchezo utakaopigwa dimba la Amaan kesho Januari 07 2019.
Mchezo huo utapigwa saa mbili na robo usiku.
Licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc, Yanga bado ina nafasi ya kutinga nusu fainali kutoka kundi B kama itafanya vizuri katika michezo yake miwili iliyobaki kukamilisha hatua ya makundi.
ADVERTISE HERE