Yanga imemaliza michuano ya kombe la Mapinduzi kibabe baada ya kuichapa Jamhuri Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa dimba la Amaani Jumatano jioni.
Jamhuri Fc ilitangulia kufunga mapema kwenye dakika ya tatu kupitia kwa Khalfan Swaleh kabla Faraji Kilaza hajaisawazishia Yanga kwenye dakika ya 20 na Shaban Mohammed na Pius Buswita kuongeza mabao mawili katika dakika za 28 na 32.
Yanga imemaliza nafasi ya tatu kundi B nyuma ya Azam Fc na Malindi ikiwa imejikusanyia alama sita baada ya kushuka dimbani mara nne.
Imeshinda michezo miwili na kupoteza michezo miwili.
Azam Fc na Malindi zimejihakikishia kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili kundi B
ADVERTISE HERE