Uongozi wa Yanga umeweka wazi dhamira yake ya kuwania mataji mawili msimu huu, Ligi Kuu na kombe la FA (ASFC)
Baada ya Yanga kupangwa na Biashara Fc kwenye mchezo wa raundi ya nne kombe la FA, msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema watajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo huo utakaopigwa kati ya Jan 25-28
Ten amesema wameipa kipaumbele michuano hiyo na wamedhamiria kutwaa ubingwa
Kama Yanga itashinda mchezo huo, raundi ya tano itacheza na mshindi kati ya Almighty Elephant dhidi ya Namungo Fc katika mchezo ambao mshindi atatinga robo fainali
Kwa upande wa ligi kuu Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili
Baada ya kumaliza mzunguuko wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, uongozi wa timu hiyo umepania kuendeleza mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa kuhakikisha timu inatwaa ubingwa.
Moja ya sababu iliyopelekea kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kupeleka kikosi cha vijana kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, ni kuhakikisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza wanapata mapumziko ya kutosha kabla ya kuanza mikikimikiki ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi msimu huu