Mkemi atangaza kurudi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2019
Mkemi atangaza kurudi Yanga

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Salum Mkemi ambaye alijiuzulu nafasi yake mwaka jana, ametangaza kurudi katika nafasi hiyo baada ya barua yake ya kujiuzulu kutojibiwa na uongozi wa Yanga.

Kulingana na taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayodaiwa kutolewa na Mkemi, amesema amerudi rasmi katika nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuanzia leo Ijumaa, Januari 11, 2019 baada ya barua yake ya kujiuzulu kukosa majibu

Aidha Mkemi amesema viongozi waliopo Yanga kwa sasa hawatoshi (akidi) kuijadili barua hiyo hivyo ameamua kurudi katika majukumu yake katika Kamati ya Utendaji ya Yanga

Mkemi amefikia uamuzi huo muda mfupi baada ya TFF kutangaza kusitisha uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga baada ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuuzuia uchaguzi Mahakamani.

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike keshokutwa, Januari 13, 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
54m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’