Mshambuliaji kinara wa mabao ligi kuu ya Tanzania Bara Heritier Makambo huenda akaukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui Fc
Kulingana na mtandao wa DaboTen, Makambo ametoweka katika Hotel aliyofikia na hajulikani aliko
Mtandao huo umeeleza kuwa kinara huyo wa mabao aliyeifungia Yanga mabao 11, ametoweka katika Hotel hiyo aliyokuwa akiishi pamoja na mizigo yake yote.
Awali ilielezwa Makambo alikuwa amepewa mapumziko na alitarajiwa kurejea leo kutoka DR Congo
Kweli Makambo hayupo - Ten
Msemaji wa Yanga Dismas Ten amekiri kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo hajarejea kutoka DR Congo alikokwenda kwa ajili ya mapumziko na hapatikani kwenye simu
ADVERTISE HERE