Takwimu bado zinaibeba Yanga mbio za ubingwa msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2017
Takwimu bado zinaibeba Yanga mbio za ubingwa msimu huu
Wapo waliokata tamaa baada ya matokeo ya mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom kwa mabingwa watetezi Yanga kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lipuli.

Ukweli ni kwamba katika misimu saba iliyopita, Yanga imetwaa taji la VPL mara nyingi pale inapoanza kwa sare au kufungwa kuliko ilivyoanza kwa ushindi.

Katika kipindi hicho, haikushinda katika mechi tatu za ufunguzi, lakini ni mara moja tu ndio haikutwa taji.

Yanga ilianza msimu wa 2012/13 vibaya kwa kupata suluhu na Prisons ya Mbeya, lakini baadaye iliweka mitambo sawa na kutwaa ubingwa.

Msimu wa 2014/15 pia iliuanza vibaya ikichapwa 2-0 na Mtibwa Sugar, lakini baadaye iliweka mambo sawa na kutwaa ubingwa.

Msimu ambao Yanga ilianza vibaya na kupoteza ubingwa ni 2011/12 ambao ilifungwa bao 1-0 na JKT Ruvu. Simba ilishinda taji.

Msimu uliopita pia Yanga ilikuwa na mwendo wa kusuasua mwanzoni tena msimu huo ulikuwa mgumu sana maana kuna kipindi Yanga ilikuwa imeachwa nyuma kwa pointi tisa na Simba.

Lakini mwishoni mwa msimu Yanga ikatwaa ubingwa na kupelekea taharuki kwa Simba hadi kugoma kupokea zawadi ya mshindi wa pili wakidai kusubiri pointi za FIFA.

Kwa upande wa Simba, licha ya kutopoteza mchezo wa ufunguzi katika miaka saba iliyopita, imeshinda ubingwa mara moja tu, 2012.

Matokeo mabaya ya mechi za ufunguzi kwa Simba katika kipindi hicho ni sare ya 2-2 na Rhino Rangers (2013) na sare kama hiyo dhidi ya Coastal Union mwaka 2014.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’