Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo wanashuka katika dimba la Taifa kuikabili Kariaobang Sharks kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup
Mchezo huo utapigwa saa kumi na robo jioni. Mchezo wa mapema utakaopigwa saa nane mchana ni kati ya Singida United dhidi ya Bandari Fc
Yanga inashiriki michuano hiyo kwa mara ya tatu.
Katika msimu wa kwanza michuano hiyo ilipofanyika jijini Dar es salaam Yanga ilitolewa katika hatua ya nusu fainali na mwaka jana ilipofanyika nchini Kenya Yanga ilitolewa hatua ya kwanza ya robo fainali
Hata hivyo msimu huu Yanga imeyapa kipaumbele mashindano hayo tofauti na misimu miwili iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema leo anatarajiwa kushusha kikosi chake cha kwanza
Zahera alisema malengo waliyojiwekea katika michuano hiyo ni kutwaa ubingwa
Michezo ya michuano hiyo ni ya mtoano hivyo mshindi ni lazima apatikane katika kila mchezo. Kama mchezo utamalizika kwa matokeo ya sare, changamoto ya mikwaju ya penati itatumika kumpata mshindi