Mwafaka kuhusu Beno uko karibu kupatikana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2019
Mwafaka kuhusu Beno uko karibu kupatikana

Taarifa zilizopatikana mapema leo zimebainisha kuwa majadiliano ya kumrejesha Beno Kakolanya kikosini yanaendelea na upo uwezekano mkubwa mwafaka utafikiwa

Yanga imedhamiria kutwaa ubingwa msimu huu, inahitaji kuwa imara katika kila idara ili kulifanikisha hilo

Licha ya Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki kuendelea kuibeba Yanga iliyopoteza mchezo mmoja tu tangu Kakolanya alipogoma, uzoefu wa mlinda lango huyo huenda ukahitajika katika mzunguuko huu wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Hivi karibuni Mwanasheria wa Beno alikutana na uongozi wa Yanga kuutaka umwachie huru mlinda lango huyo kwa kuvunja mkataba wake, kwani kuendelea kumn'gan'gania wakati hawamtumii ni kumuharibia kipaji chake

Kwa kipindi chote ambacho Kakolanya amekosekana katika kikosi cha Yanga atakuwa amejifunza jambo.

Kama utapatikana mwafaka basi hakuna shaka Wana Jangwani watampokea tena kwa mikono miwili

Lakini angalizo limetolewa kuwa ni muhimu Kocha Mwinyi Zahera akaridhia urejeo wake, kwani kama uongozi wa Yanga utamrudisha bila ridhaa yake, kocha huyo tayari ameshasema kuwa ataondoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’