Wiki iliyopita Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wake Malangwe Mchungahela ilitoa taarifa kuwa mchakato wa uchaguzi wa Yanga ungeendelea baada ya siku saba
Hiyo ilikuwa baada ya kufikia makubaliano na wanachama wa klabu hiyo waliokuwa wamefungua kesi Mahakamani kuridhia kuziondoa kesi hizo
Licha ya muda huo kupita, hakuna taarifa zaidi iliyotolewa kuhusu hatma ya uchaguzi huo ambao awali uliopangwa kufanyika Januari 13, 2019
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mchungahela awali, uchaguzi huo utafanyika, angetangaza tarehe ya uchaguzi baada ya siku saba huku wakitoa siku moja kwa wagombea kufanya kampeni
Kampeni zilisitishwa sambamba na uchaguzi baada ya baadhi ya Wanachama kufungua kesi Mahakamani