Mbao Fc timu pekee ya Tanzania iliyokuwa imebaki kwenye michuano ya SportPesa Cup imeyaaga mashindano hayo baada kufungwa kwa mikwaju ya penati 6-5 na K.Sharks kwenye mchezo wa nusu fainali kufuatia matokeo ya 0-0
Mbao imeungana na Simba kuwa timu za mwisho kutolewa katika michuano hiyo leo
Bandari Fc na K.Sharks zitachuana kwenye mchezo wa fainali wakati Mbao Fc na Simba zitachuana kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu
Timu za Kenya zimeendelea kutawala michuano hiyo zikijihakikishia kutwaa taji kwa msimu wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE