Mbinu za Zahera zitatupa ubingwa - Tambwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2019
Mbinu za Zahera zitatupa ubingwa - Tambwe

Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amesema chini ya kocha Mwinyi Zahera wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu kutokana na kocha huyo kuwa na mbinu nyingi

Tambwe ambaye amefunga mabao sita kwenye ligi mpaka sasa, amesema licha ya ugumu wa ligi katika mzunguuko wa pili, anaamini wataendeleza makali waliyomalizana nayo mzunguuko wa kwanza

Amesema wamesahau matokeo ya kufungwa mchezo uliopita na wanajipanga kikamilifu kuhakikisha wanatimiza lengo la kutwaa ubingwa

"Naiona nafasi ya timu yangu kufanya vizuri msimu huu, tumepoteza mchezo mmoja lakini tunaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi, tunaweza kuendeleza makali yetu," amesema.

"Tuna kocha mzuri, ana mbinu nyingi ambazo tunauhakika zitatusaidia kutwaa ubingwa msimu huu, kila mchezo kocha amekuwa akitupa mbinu za kushinda"

Tambwe amerejesha makali yake ya kuzifumania nyavu. Katika michuano ya SportPesa alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya K. Sharks uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 3-2

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Haritier Makambo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
55m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’