Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wanajiandaa kikamilifu kushinda michezo yao katika michuano yote wanayoshiriki ili kurudisha heshima ya mabingwa hao wa kihistoria Tanzania
Yanga inakabiliwa na mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Biashara United utakaopigwa katika dimba la Taifa keshokutwa, Januari 31 2019
Hafidh amesema lengo kuu ni kutwaa taji la michuano hiyo ili kujihakikishia kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao
"Kila mechi kwetu sisi ni fainali," amesema Hafidh
"Tunahitaji kushinda mchezo huu ili tusonge mbele hatua inayofuata. Msimu huu tumepania kuirejesha heshima ya Yanga, tumedhamiria kushind taji hili"
Yanga pia ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na alama 53, wanaongoza kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 20