Baada ya kupewa na mapumziko ya siku moja na kocha Mwinyi Zahera, mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amereja kikosini tayari kuikabili Coastal Union hapo kesho
Tambwe alipata jeraha juu ya jicho lililomfanya ashonwe nyuzi tano kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United uliofanyika juzi Alhamisi baada ya kugongana na mlinda lango wa timu hiyo Nurdine Barola
Tambwe leo alishiriki katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika kwenye dimba la Mkwakwani kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili katika dimba hilo la Mkwakwani
ADVERTISE HERE