Zahera alivyowashangaza 'wagosi' Tanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Feb 2019
Zahera alivyowashangaza 'wagosi' Tanga

Huyu Mwinyi Zahera achaneni naye kabisa, kwani unaambiwa kitu alichofanya Mkwakwani kimewashangaza wakazi wa jijini Tanga.

Mara baada ya kumalizika kwa pambano lao dhidi ya Coastal Union, kocha huyo kutoka DR Congo aliwafanya sapraizi walemavu wa miguu watembeleao baiskeli maalumu.

Zahera aliwaona walemavu hao wakiwa wameketi pembeni mwa uwanja baada ya kumaliza mahojiano yake na Wanahabari alimtuma shabiki mmoja awaite.

Watu wenye ulemavu wapatao watano walipokutana na Zahera alitoa Sh 100,000 kisha akawaambia hana kikubwa kaamua kugawana nao.

“Nawapenda sana na Mungu awabariki, niliwaona wengi ili mradi mmerudi wachache chukueni hiki hapa,” anafungua pochi yake na kuwapa pesa.

Mwanaspoti lilipomuuliza amekuwa akitoa mara kwa mara kwa wenye mahitaji maalumu, msukumo huo unatokana na nini! Alijibu anapokuwa nacho anaamini wengine hawana.

“Napenda kutoa sadaka kwa njia mbalimbali sijali ni mashabiki wa Yanga ama Simba kwangu ubinadamu ni jambo kubwa ni kitu kinachotoka ndani ya moyo wangu” alisema.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’