Zahera amtahadharisha JITU, amwambia 'nitakufunga jela'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2019
Zahera amtahadharisha JITU, amwambia 'nitakufunga jela'

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtahadharisha Mwanachama maarufu wa klabu ya Yanga anayefahamika zaidi kwa jina la 'Jitu' kuwa atamshitaki Mahakamani kama ataendela kufanya uchocheziΒ  na kumkashifu

Hivi karibuni Jitu akiwa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari alisema mashabiki wa Yanga watampiga mawe kocha Zahera kama hatamchezesha Beno Kakolanya kwenye mchezo dhidi ya Simba iwapo Yanga itafungwa.

Aidha Jitu aliendelea kusema Zahera amemkataa Beno kwa sababu anataka kumsaidia mlinda lango Klaus Kindoki ambaye ni nduguye kutoka Congo

Alisema uwezo wa Kindoki ni mdogo sana na ni bora akachukuliwa mkewe kudaka kwenye mchezo dhidi ya Simba kama Beno hatarudishwa

"Jitu simfahamu sijawahi kukutana nae mahali popote katika maisha yangu. Ameenda kufanya video kusema mambo ya ovyo, mambo ya upumbavu"

"Anasema Zahera yule tutampiga majiwe kama Simba anatupiga sababu hamchezeshi Beno Kakolanya. Ninamtahadharisha kwa mara ya mwisho naweza nikamfunga," amesema Zahera

Mara kwa mara Jitu amekuwa akiingia katika mgogoro na viongozi wa klabu ya Yanga

Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika mwaka jana, Jitu alitolewa katika mkutano chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kupinga baadhi ya ajenda za Mkutano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’