Kikosi cha Yanga kimeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, Februari 16 katika uwanja wa Taifa
Kuelekea michezo muhimu Yanga ina kawaida ya kuweka kambi nje ya jiji la Dar es salaam hasa kisiwani Pemba na Morogoro
Kikosi cha Yanga kilielekea mkoani Morogoro mara baada ya kumaliza mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa juzi katika dimba la Mkwakwani na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atakuwa na nafasi ya kuwaandaa vijana wake tayari kuwavaa Simba kwenye mchezo wa pili msimu huu
Katika mchezo wa duru ya kwanza ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Yanga iliweka kambi mkoani Morogoro pia
ADVERTISE HERE