Yanga inaelekea mkoani Mwanza leo ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi wa benchi la Ufundi tayari kuikabili Mbao Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa katika dimba la CCM Kirumba keshokutwa, Februari 20 2019
Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' na mlinzi wa pembeni Gadiel Michael hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kinachokwenda Mwanza kwa kuwa wana kadi tatu za njano
Gadiel na Fei Toto walionyeshwa kadi za njano juzi katika mchezo dhidi ya Simba
kikosi kinachosafiri;
Ramadhani Kabwili, Paul Godfrey, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu, Mohamed Issa, Papy Tshishimbi, Heritier Makambo, Amissi Tambwe, Ibrahim Ajib, Klaus Kindoki, Juma Abdul, Haruna Moshi, Mrisho Ngasa, Matheo Antony, Deus Kaseke, Raphael Daud, Jaffar Mohammed na Said Makapu.