Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema hakukuwahi kuwa na tofauti yoyote kati ya nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib na beki kisiki Kelvin Yondani
Katika mchezo wa watani wa jadi uliopigwa mwishoni mwa wiki, iliripotiwa kuwa Yondani aligoma kumpa mkono Ajib tukio lililotafsiriwa kuwa wawili hao hawapatani
Hata hivyo Ajib na Yondani wako jijini Mwanza na kikosi cha Yanga ambapo jana walionekana wakitaniana na kufurahi pamoja
"Hakuna tatizo wala tofauti yeyote iliopo wala iliowahi kuwepo kati ya hawa vijana wetu wawili @kelvinyondan5 na nahodha wetu @ibrahimajibu23 kama ambavyo inaenezwa kwenye mitandao ya kijamii," Hafidh amesema
Juzi Ajib alitoa ufafanuzi wa kilichotokea siku hiyo ambapo alisema wachezaji wenzie walishangazwa na utaratibu alioutumia wa kuwapa mkono wakati akiwatambulisha kwa mgeni rasmi, hali iliyopelekea baadhi kutompa mkono