FT : Mbao Fc 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2019
FT : Mbao Fc 1-2 Yanga

Yanga imefuta uteja kwa Mbao Fc ndani ya dimba la CCM Kirumba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa leo

Mbao Fc ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 45 likiwekwa kambani kwa kichwa na Robert Ndaki

Yanga iliyouanza mchezo huo taratibu ilibadilika katika kipindi cha pili kwa kupeleka mashambulizi ya nguvu langoni kwa Mbao Fc

Heritier Makambo aliirudisha Yanga mchezoni kwenye dakika ya 50 akimalizia kwa kichwa krosi murua iliyochongwa na Papi Tshishimbi

Yanga iliendelea kupeleka mashambulizi langoni kwa Mbao Fc na iliandika bao la pili kwenye dakika ya 68 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Amissi Tambwe

Penati hiyo ilikuwa ni zao la shambulizi la kushitukiza lililofanywa na Yanga ambapo krosi ya beki Kelvin Yondani aliyekuwa amepanda ilitua mkononi mwa mlinzi wa Mbao Fc ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru upigwe mkwaju wa penati

Ushindi huo umeendelea kuikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imefikisha alama 61

Makambo amerudi kileleni mwa orodha ya wapachika mabao akifikisha mabao 12 sawa na Salum Aiyee wa Mwadui Fc

Tambwe amefunga bao lake la saba leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’